Akeelah – Nipende Pende Lyrics

SHIRKO, Shirko Media

Moyo wangu pale ukiungana na macho
Nikikutazama wewe wengine sioni kitu
Najiwazia wazia niwe mama kijacho
Nizae na wewe wengine wasidhubutu

Nawakataa wale wanaonikatia katia
Niwe na wewe, mwanamume unayenijulia
Nawe jiepushe na wale wa kuvamia vamia
Ndio maana kwako nimetulia

Basi nipende pende, ah wewe
Unipe peremende, ah wewe
Usichoke nibemende
Baridi ya mande nisikie sikie

Nipende pende, ah wewe
Nipe lozi na tende, ah wewe
Basi nigande gande
Usiniache baby wangu

I love you, nimejichimba chimba
I feel you, ndio maana navimba
I love you, nimejichimba chimba
I feel you, ndio maana navimba

Nimekuruhusu uniweke kwenye kiganja
Maana kwenye penzi langu sina ujanja
Ndani ya moyo jina lako nimejichanja
Wasio tupenda nyuso wamezikunja

Basi nibebe
Nimemiss mlingoti dedede
Nyumbani weka sengenge
Manyaku nyaku mje kuwazuia

Tamu zege zege
Mahaba ya juu kama ndege
Wasitutie na dege
Mwisho wake wakatuharibia

Basi nipende pende, ah wewe
Unipe peremende, ah wewe
Usichoke nibemende
Baridi ya mande nisikie sikie

Nipende pende, ah wewe
Nipe lozi na tende, ah wewe
Basi nigande gande
Usiniache baby wangu

I love you, nimejichimba chimba
I feel you, ndio maana navimba
I love you, nimejichimba chimba
I feel you, ndio maana navimba

Ukiwa mbali
Wasi wasi ndio unazidi
Nina wivu silali
Na kukera ndio sina budi

Nakumbuka mbali
Kukulale ua kifudi fudi
Siishi visababu
Mwenzio natamani urudi baby